previous next

Mathayo 5

Hotuba mlimani

1 Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea, 2 naye akaanza kuwafundisha:

Furaha ya kweli

(Luka 6:20-23)

3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

5  t Heri walio wapole, maana watairithi nchi.

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

7 Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.

8  t Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.

9 Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.

10 Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

11 “Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. 12 Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.

Chumvi na mwanga

Marko 9:50; Luka 14:34-35

13 “Nyinyi ni chumvi ya dunia. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.

14 “Nyinyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika. 15 Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani. 16 Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Kuhusu sheria

17 “Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha. 18 Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia. 19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Kuhusu hasira

(Luka 12:57-59)

21 “Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: ‘Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.’ 22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: ‘Pumbavu’ atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.

23 “Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, 24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi utoe sadaka yako.

25 “Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani. 26 Kweli nakuambia, hutatoka humo mpaka umelipa senti ya mwisho.

Kuhusu uzinzi

27 “Mmesikia kwamba watu waliambiwa: ‘Usizini!’ 28 Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake. 29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, lingoe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu. 30 Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.

Kuhusu talaka

(Mat 19:9; Marko 10:11-12; Luka 16:18)

31 “Ilikwisha semwa pia: ‘Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka’. 32 Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

Kuhusu kiapo

33 “Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’ 34 Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu; 35 t wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema, ‘Ndiyo’, basi iwe ‘Ndiyo’; ukisema, ‘Siyo’, basi iwe kweli ‘Siyo’. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.

Kuhusu kulipiza kisasi

(Luka 6:29-30)

38 “Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Jicho kwa jicho, jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili. 40 Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako. 41 Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili. 42 Akuombaye mpe, wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu.

Kuwapenda maadui

(Luka 6:27-28,32-36)

43 “Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Mpende jirani yako, na kumchukia adui yako.’ 44 Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu. 46 Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo! 47 Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo. 48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Matthew 5

1 And seeing the multitudes, he went up into the mountain: and when he had sat down, his disciples came unto him:2 and he opened his mouth and taught them, saying,

3 Blessed are the poor in spirit: for theirs is the kingdom of heaven.

4 Blessed are they that mourn: for they shall be comforted.

5 Blessed are the meek: for they shall inherit the earth.

6 Blessed are they that hunger and thirst after righteousness: for they shall be filled.

7 Blessed are the merciful: for they shall obtain mercy.

8 Blessed are the pure in heart: for they shall see God.

9 Blessed are the peacemakers: for they shall be called sons of God.

10 Blessed are they that have been persecuted for righteousness’ sake: for theirs is the kingdom of heaven.11 Blessed are ye when men shall reproach you, and persecute you, and say all manner of evil against you falsely, for my sake.12 Rejoice, and be exceeding glad: for great is your reward in heaven: for so persecuted they the prophets that were before you.

13 Ye are the salt of the earth: but if the salt have lost its savor, wherewith shall it be salted? it is thenceforth good for nothing, but to be cast out and trodden under foot of men.14 Ye are the light of the world. A city set on a hill cannot be hid.15 Neither do men light a lamp, and put it under the bushel, but on the stand; and it shineth unto all that are in the house.16 Even so let your light shine before men; that they may see your good works, and glorify your Father who is in heaven.

17 Think not that I came to destroy the law or the prophets: I came not to destroy, but to fulfil.18 For verily I say unto you, Till heaven and earth pass away, one jot or one tittle shall in no wise pass away from the law, till all things be accomplished.19 Whosoever therefore shall break one of these least commandments, and shall teach men so, shall be called least in the kingdom of heaven: but whosoever shall do and teach them, he shall be called great in the kingdom of heaven.20 For I say unto you, that except your righteousness shall exceed the righteousness of the scribes and Pharisees, ye shall in no wise enter into the kingdom of heaven.

21 Ye have heard that it was said to them of old time, Thou shalt not kill; and whosoever shall kill shall be in danger of the judgment:22 but I say unto you, that every one who is angry with his brother shall be in danger of the judgment; and whosoever shall say to his brother, Raca, shall be in danger of the council; and whosoever shall say, Thou fool, shall be in danger of the hell of fire.23 If therefore thou art offering thy gift at the altar, and there rememberest that thy brother hath aught against thee,24 leave there thy gift before the altar, and go thy way, first be reconciled to thy brother, and then come and offer thy gift.25 Agree with thine adversary quickly, while thou art with him in the way; lest haply the adversary deliver thee to the judge, and the judge deliver thee to the officer, and thou be cast into prison.26 Verily I say unto thee, thou shalt by no means come out thence, till thou have paid the last farthing.

27 Ye have heard that it was said, Thou shalt not commit adultery:28 but I say unto you, that every one that looketh on a woman to lust after her hath committed adultery with her already in his heart.29 And if thy right eye causeth thee to stumble, pluck it out, and cast it from thee: for it is profitable for thee that one of thy members should perish, and not thy whole body be cast into hell.30 And if thy right hand causeth thee to stumble, cut it off, and cast it from thee: for it is profitable for thee that one of thy members should perish, and not thy whole body go into hell.31 It was said also, Whosoever shall put away his wife, let him give her a writing of divorcement:32 but I say unto you, that every one that putteth away his wife, saving for the cause of fornication, maketh her an adulteress: and whosoever shall marry her when she is put away committeth adultery.

33 Again, ye have heard that it was said to them of old time, Thou shalt not forswear thyself, but shalt perform unto the Lord thine oaths:34 but I say unto you, swear not at all; neither by the heaven, for it is the throne of God;35 nor by the earth, for it is the footstool of his feet; nor by Jerusalem, for it is the city of the great King.36 Neither shalt thou swear by thy head, for thou canst not make one hair white or black.37 But let your speech be, Yea, yea; Nay, nay: and whatsoever is more than these is of the evil one.

38 Ye have heard that it was said, An eye for an eye, and a tooth for a tooth:39 but I say unto you, resist not him that is evil: but whosoever smiteth thee on thy right cheek, turn to him the other also.40 And if any man would go to law with thee, and take away thy coat, let him have thy cloak also.41 And whosoever shall compel thee to go one mile, go with him two.42 Give to him that asketh thee, and from him that would borrow of thee turn not thou away.

43 Ye have heard that it was said, Thou shalt love thy neighbor, and hate thine enemy:44 but I say unto you, love your enemies, and pray for them that persecute you;45 that ye may be sons of your Father who is in heaven: for he maketh his sun to rise on the evil and the good, and sendeth rain on the just and the unjust.46 For if ye love them that love you, what reward have ye? do not even the publicans the same?47 And if ye salute your brethren only, what do ye more than others? do not even the Gentiles the same?48 Ye therefore shall be perfect, as your heavenly Father is perfect.