FLP. 2
Kuiga Unyenyekevu wa Kristo
1 Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, 2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. 3 tMsitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 4 tKila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. 5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 tambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 tbali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 ttena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9 tKwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 tili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.Kuangaza kama Mianga Ulimwenguni
12 tBasi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 tKwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
14 tYatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, 15 tmpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, 16 tmkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure. 17 tNaam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
18 tNanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.Timotheo na Epafrodito
19 Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 20 tMaana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 21 tMaana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. 22 Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake. 23 Basi, natumaini kumtuma huyo mara, hapo nitakapojua yatakayonipata.
24 tNami naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe hivi karibu.
25 tLakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu. 26 Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi. 27 Kwa maana alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni. 28 Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu. 29 tMpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa. 30 Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake; ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu.
PHILIPPIANS 2
True Humility
1 Christ encourages you, and his love comforts you. God's Spirit unites you, and you are concerned for others. 2 Now make me completely happy! Live in harmony by showing love for each other. Be united in what you think, as if you were only one person. 3 Don't be jealous or proud, but be humble and consider others more important than yourselves. 4 Care about them as much as you care about yourselves
5 and think the same way that Christ Jesus thought:t
6 Christ was truly God.
But he did not try to remaint
equal with God.
7 Instead he gave up everythingt
and became a slave,
when he became
like one of us.
8 Christ was humble.
He obeyed God and even died
on a cross.
9 Then God gave Christ
the highest place
and honored his name
above all others.
10 t So at the name of Jesus
everyone will bow down,
those in heaven, on earth,
and under the earth.
11 And to the glory
of God the Father
everyone will openly agree,
“Jesus Christ is Lord!”Lights in the World
12 My dear friends, you always obeyed when I was with you. Now that I am away, you should obey even more. So work with fear and trembling to discover what it really means to be saved.
13 God is working in you to make you willing and able to obey him.
14 Do everything without grumbling or arguing. 15 t Then you will be the pure and innocent children of God. You live among people who are crooked and evil, but you must not do anything they can say is wrong. Try to shine as lights among the people of this world,
16 as you hold firmly tot the message that gives life. Then on the day when Christ returns, I can take pride in you. I can also know that my work and efforts were not useless.
17 Your faith in the Lord and your service are like a sacrifice offered to him. And my own blood may have to be poured out with the sacrifice.t If this happens, I will be glad and rejoice with you.
18 In the same way, you should be glad and rejoice with me.Timothy and Epaphroditus
19 I want to be encouraged by news about you. So I hope the Lord Jesus will soon let me send Timothy to you. 20 I don't have anyone else who cares about you as much as he does. 21 The others think only about what interests them and not about what concerns Christ Jesus. 22 But you know what kind of person Timothy is. He has worked with me like a son in spreading the good news. 23 I hope to send him to you, as soon as I find out what is going to happen to me.
24 And I feel sure the Lord will also let me come soon.
25 I think I ought to send my dear friend Epaphroditus back to you. He is a follower and a worker and a soldier of the Lord, just as I am. You sent him to look after me, 26 but now he is eager to see you. He is worried, because you heard he was sick.
27 In fact, he was very sick and almost died. But God was kind to him, and also to me, and he kept me from being burdened down with sorrow.
28 Now I am more eager than ever to send Epaphroditus back again. You will be glad to see him, and I won't have to worry any longer. 29 Be sure to give him a cheerful welcome, just as people who serve the Lord deserve. 30 He almost died working for Christ, and he risked his own life to do for me what you could not.