previous next

UFU. 16

Ghadhabu ya Mungu

1  tNikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.

2  tAkaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.

3  tNa huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
4  tNa huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. 5 tNami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; 6 tkwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.

7 tNikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako.
8 Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.

9 tWanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.
10  tNa huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,

11 twakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao.
12  tNa huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13 tNikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 tHizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 t(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)

16 tWakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.
17  tNa huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. 18 tPakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 19 tNa mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20 tKila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 21 tNa mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

REVELATION 16

The Bowls of God's Anger

1 From the temple I heard a voice shout to the seven angels, “Go and empty the seven bowls of God's anger on the earth.”

2  t The first angel emptied his bowl on the earth. At once ugly and painful sores broke out on everyone who had the mark of the beast and worshiped the idol.

3 The second angel emptied his bowl on the sea. At once the sea turned into blood like that of a dead person, and every living thing in the sea died.
4  t The third angel emptied his bowl into the rivers and streams. At once they turned to blood.

5 Then I heard the angel, who has power over water, say,
“You have always been,
and you always will be
the holy God.
You had the right
to judge in this way.

6 They poured out the bloodt
of your people
and your prophets.
So you gave them blood
to drink as they deserve!”

7 After this, I heard
the altar shout,
“Yes, Lord God All-Powerful,
your judgments are honest
and fair.”
8 The fourth angel emptied his bowl on the sun, and it began to scorch people like fire.

9 Everyone was scorched by its great heat, and all of them cursed the name of God who had power over these terrible troubles. But no one turned to God and praised him.
10  t The fifth angel emptied his bowl on the throne of the beast. At once darkness covered its kingdom, and its people began biting their tongues in pain.

11 And because of their painful sores, they cursed the God who rules in heaven. But still they did not stop doing evil things.
12  t The sixth angel emptied his bowl on the great Euphrates River, and it completely dried up to make a road for the kings from the east. 13 An evil spirit that looked like a frog came out of the mouth of the dragon. One also came out of the mouth of the beast, and another out of the mouth of the false prophet.

14 These evil spirits had the power to work miracles. They went to every king on earth, to bring them together for a war against God All-Powerful. But that will be the day of God's great victory.

15  t Remember Christ says, “When I come, it will surprise you like a thief! But God will bless you, if you are awake and ready. Then you won't have to walk around naked and be ashamed.”

16  t Those armies came together in a place that in Hebrew is called Armagedon.t
17 As soon as the seventh angel emptied his bowl in the air, a loud voice from the throne in the temple shouted, “It's done!” 18 t There were flashes of lightning, roars of thunder, and the worst earthquake in all history. 19 t The great city of Babylon split into three parts, and the cities of other nations fell. So God made Babylon drink from the wine cup filled with his anger. 20 t Every island ran away, and the mountains disappeared. 21 t Hailstones, weighing about 50 kilograms each, fell from the sky on people. Finally, the people cursed God, because the hail was so terrible.