UFU. 20
Miaka Elfu Moja
1 tKisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 tAkamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3 takamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
4 tKisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 tHao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
6 tHuo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.Kuangamizwa kwa Shetani
7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 tnaye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 tWakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
10 tNa yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.Wafu Wahukumiwa
11 tKisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 tNikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 tBahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 tMauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 tNa iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
REVELATION 20
The Thousand Years
1 I saw an angel come down from heaven, carrying the key to the deep pit and a big chain. 2 t He chained the dragon for 1,000 years. It is that old snake, who is also known as the devil and Satan.
3 Then the angel threw the dragon into the pit. He locked and sealed it, so 1,000 years would go by before the dragon could fool the nations again. But after that, it would have to be set free for a little while.
4 t I saw thrones, and sitting on those thrones were the ones who had been given the right to judge. I also saw the souls of the people who had their heads cut off because they had told about Jesus and preached God's message. They were the same ones who had not worshiped the beast or the idol, and they had refused to let its mark be put on their foreheads or hands. They will come to life and rule with Christ for 1,000 years.
5-6 These people are the first to be raised to life, and they are especially blessed and holy. The second deatht has no power over them. They will be priests for God and Christ and will rule with them for 1,000 years.
No other dead people were raised to life until 1,000 years later.Satan Is Defeated
7 At the end of the 1,000 years, Satan will be set free. 8 t He will fool the countries of Gog and Magog, which are at the far ends of the earth, and their people will follow him into battle. They will have as many followers as there are grains of sand along the beach, 9 and they will march all the way across the earth. They will surround the camp of God's people and the city God loves. But fire will come down from heaven and destroy the whole army.
10 Then the devil who fooled them will be thrown into the lake of fire and burning sulfur. He will be there with the beast and the false prophet, and they will be in pain day and night forever and ever.The Judgment //at the Great White Throne
11 t I saw a great white throne with someone sitting on it. Earth and heaven tried to run away, but there was no place for them to go.
12 t I also saw all the dead people standing in front of that throne. Every one of them was there, no matter who they had once been. Several books were opened, and then the book of lifet was opened. The dead were judged by what those books said they had done.
13 The sea gave up the dead people who were in it, and death and its kingdom also gave up their dead. Then everyone was judged by what they had done. 14 Afterwards, death and its kingdom were thrown into the lake of fire. This is the second death.t 15 Anyone whose name wasn't written in the book of life was thrown into the lake of fire.