previous next

UFU. 4

Ibada ya Mbinguni

1  tBaada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. 2 tNa mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti; 3 tna yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi. 4 tNa viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. 5 tNa katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu. 6 ttNa mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. 7 tNa huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye. 8 tNa hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja. 9 tNa hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele, 10 tndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema, 11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.

REVELATION 4

Worship in Heaven

1 After this, I looked and saw a door that opened into heaven. Then the voice that had spoken to me at first and that sounded like a trumpet said, “Come up here! I will show you what must happen next.” 2 t Right then the Spirit took control of me, and there in heaven I saw a throne and someone sitting on it.

3 The one who was sitting there sparkled like precious stones of jaspert and carnelian.t A rainbow that looked like an emeraldt surrounded the throne.
4 Twenty-four other thrones were in a circle around that throne. And on each of these thrones there was an elder dressed in white clothes and wearing a gold crown. 5 t Flashes of lightning and roars of thunder came out from the throne in the center of the circle. Seven torches, which are the seven spirits of God, were burning in front of the throne.

6 t t Also in front of the throne was something that looked like a glass sea, clear as crystal.
Around the throne in the center were four living creatures covered front and back with eyes.
7 The first creature was like a lion, the second one was like a bull, the third one had the face of a human, and the fourth was like a flying eagle.

8 t Each of the four living creatures had six wings, and their bodies were covered with eyes. Day and night they never stopped singing,
“Holy, holy, holy is the Lord,
the all-powerful God,
who was and is
and is coming!”
9 The living creatures kept praising, honoring, and thanking the one who sits on the throne and who lives forever and ever.

10 At the same time the 24 elders knelt down before the one sitting on the throne. And as they worshiped the one who lives forever, they placed their crowns in front of the throne and said,

11  t “Our Lord and God,
you are worthy
to receive glory,
honor, and power.
You created all things,
and by your decision they are
and were created.”