RUM. 12
Maisha Mapya katika Kristo
1 tBasi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 tWala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
3 tKwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. 4 tKwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 tVivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 tBasi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; 7 tikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8 tmwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.Sifa za Mkristo
9 tPendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. 10 tKwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; 11 tkwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; 12 tkwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; 13 tkwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. 14 tWabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. 15 tFurahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. 16 tMpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili. 17 tMsimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 tKama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. 19 tWapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20 tLakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
ROMANS 12
Christ Brings New Life
1 Dear friends, God is good. So I beg you to offer your bodies to him as a living sacrifice, pure and pleasing. That's the most sensible way to serve God.
2 Don't be like the people of this world, but let God change the way you think. Then you will know how to do everything that is good and pleasing to him.
3 I realize God has treated me with undeserved grace, and so I tell each of you not to think you are better than you really are. Use good sense and measure yourself by the amount of faith that God has given you. 4 t A body is made up of many parts, and each of them has its own use.
5 That's how it is with us. There are many of us, but we each are part of the body of Christ, as well as part of one another.
6 t God has also given each of us different gifts to use. If we can prophesy, we should do it according to the amount of faith we have. 7 If we can serve others, we should serve. If we can teach, we should teach.
8 If we can encourage others, we should encourage them. If we can give, we should be generous. If we are leaders, we should do our best. If we are good to others, we should do it cheerfully.Rules for Christian Living
9 Be sincere in your love for others. Hate everything that is evil and hold tight to everything that is good. 10 Love each other as brothers and sisters and honor others more than you do yourself. 11 Never give up. Eagerly follow the Holy Spirit and serve the Lord. 12 Let your hope make you glad. Be patient in time of trouble and never stop praying.
13 Take care of God's needy people and welcome strangers into your home.
14 t Ask God to bless everyone who mistreats you. Ask him to bless them and not to curse them. 15 t When others are happy, be happy with them, and when they are sad, be sad. 16 t Be friendly with everyone. Don't be proud and feel that you know more than others. Make friends with ordinary people.t 17 Don't mistreat someone who has mistreated you. But try to earn the respect of others,
18 and do your best to live at peace with everyone.
19 t Dear friends, don't try to get even. Let God take revenge. In the Scriptures the Lord says,
“I am the one to take revenge
and pay them back.”
20 t The Scriptures also say,
“If your enemies are hungry,
give them something to eat.
And if they are thirsty,
give them something
to drink.
This will be the same
as piling burning coals
on their heads.”
21 Don't let evil defeat you, but defeat evil with good.