RUM. 13
Kutii Mamlaka
1 tKila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 tKwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 tkwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 6 tKwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.
7 tWapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.Upendo
8 tMsiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. 9 tMaana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
10 tPendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.Ombi la Dharura
11 tNaam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini 12 tUsiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 13 tKama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 tBali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.
ROMANS 13
Obey Rulers
1 t Obey the rulers who have authority over you. Only God can give authority to anyone, and he puts these rulers in their places of power. 2 People who oppose the authorities are opposing what God has done, and they will be punished. 3 Rulers are a threat to evil people, not to good people. There is no need to be afraid of the authorities. Just do right, and they will praise you for it.
4 After all, they are God's servants, and it is their duty to help you.
If you do something wrong, you ought to be afraid, because these rulers have the right to punish you. They are God's servants who punish criminals to show how angry God is.
5 But you should obey the rulers because you know it is the right thing to do, and not just because of God's anger.
6 t You must also pay your taxes. The authorities are God's servants, and it is their duty to take care of these matters.
7 Pay all that you owe, whether it is taxes and fees or respect and honor.Love
8 Let love be your only debt! If you love others, you have done all that the Law demands. 9 t In the Law there are many commands, such as, “Be faithful in marriage. Do not murder. Do not steal. Do not want what belongs to others.” But all of these are summed up in the command that says, “Love others as much as you love yourself.”
10 No one who loves others will harm them. So love is all that the Law demands.The Day //When Christ Returns
11 You know what sort of times we live in, and so you should live properly. It is time to wake up. You know that the day when we will be saved is nearer now than when we first put our faith in the Lord. 12 Night is almost over, and day will soon appear. We must stop behaving as people do in the dark and be ready to live in the light. 13 So behave properly, as people do in the day. Don't go to wild parties or get drunk or be vulgar or indecent. Don't quarrel or be jealous. 14 Let the Lord Jesus Christ be as near to you as the clothes you wear. Then you won't try to satisfy your selfish desires.