RUM. 5
Matokeo ya Kuhesabiwa kuwa Haki
1 tBasi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, 2 tambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. 3 tWala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; 4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; 5 tna tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. 6 Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. 7 Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. 8 tBali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 9 tBasi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. 10 tKwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
11 Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.Adamu na Kristo
12 tKwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; 13 tmaana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; 14 twalakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. 15 Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. 16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. 17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. 18 tBasi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 19 tKwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. 20 tLakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; 21 tili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.
ROMANS 5
What It Means //To Be Acceptable //to God
1 By faith we have been made acceptable to God. And now, thanks to our Lord Jesus Christ, we have peacet with God. 2 Christ has also introduced ust to God's gift of undeserved grace on which we now take our stand. So we are happy, as we look forward to sharing in the glory of God. 3 But that's not all! We gladly suffer, t because we know that suffering helps us to endure. 4 And endurance builds character, which gives us a hope
5 that will never disappoint us. All of this happens because God has given us the Holy Spirit, who fills our hearts with his love.
6 Christ died for us at a time when we were helpless and sinful. 7 No one is really willing to die for an honest person, though someone might be willing to die for a truly good person.
8 But God showed how much he loved us by having Christ die for us, even though we were sinful.
9 But there is more! Now that God has accepted us because Christ sacrificed his life's blood, we will also be kept safe from God's anger. 10 Even when we were God's enemies, he made peace with us, because his Son died for us. Yet something even greater than friendship is ours. Now that we are at peace with God, we will be saved by the life of his Son.
11 And in addition to everything else, we are happy because God sent our Lord Jesus Christ to make peace with us.Adam and Christ
12 t Adam sinned, and that sin brought death into the world. Now everyone has sinned, and so everyone must die. 13 Sin was in the world before the Law came. But no record of sin was kept, because there was no Law.
14 Yet death still had power over all who lived from the time of Adam to the time of Moses. This happened, though not everyone disobeyed a direct command from God, as Adam did.
In some ways Adam is like Christ who came later.
15 But the gift of God's undeserved grace was very different from Adam's sin. That one sin brought death to many others. Yet in an even greater way, Jesus Christ alone brought God's gift of undeserved grace to many people.
16 There is a lot of difference between Adam's sin and God's gift. That one sin led to punishment. But God's gift made it possible for us to be acceptable to him, even though we have sinned many times.
17 Death ruled like a king because Adam had sinned. But that cannot compare with what Jesus Christ has done. God has treated us with undeserved grace, and he has accepted us because of Jesus. And so we will live and rule like kings.
18 t Everyone was going to be punished because Adam sinned. But because of the good thing that Christ has done, God accepts us and gives us the gift of life.
19 Adam disobeyed God and caused many others to be sinners. But Jesus obeyed him and will make many people acceptable to God.
20 The Law came, so that the full power of sin could be seen. Yet where sin was powerful, God's gift of undeserved grace was even more powerful. 21 Sin ruled by means of death. But God's gift of grace now rules, and God has accepted us because of Jesus Christ our Lord. This means that we will have eternal life.