RUM. 6
Kufa na Kufufuka pamoja na Kristo
1 tTuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 tHasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? 3 tHamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 tBasi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 5 tKwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 6 tmkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; 7 tkwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. 8 Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; 9 tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. 10 tMaana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.
11 tVivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
12 tBasi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; 13 twala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.
14 tKwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.Watumwa wa Kutenda Haki
15 tNi nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! 16 tHamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. 17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; 18 tna mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki. 19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. 20 Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. 21 tNi faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. 22 tLakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. 23 tKwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
ROMANS 6
Dead to Sin but Alive //because of Christ
1 What should we say? Should we keep on sinning, so that God's gift of undeserved grace will show up even better? 2 No, we should not! If we are dead to sin, how can we go on sinning? 3 Don't you know that all who share in Christ Jesus by being baptized also share in his death?
4 t When we were baptized, we died and were buried with Christ. We were baptized, so we would live a new life, as Christ was raised to life by the glory of God the Father.
5 If we shared in Jesus' death by being baptized, we will be raised to life with him. 6 We know that the persons we used to be were nailed to the cross with Jesus. This was done, so our sinful bodies would no longer be the slaves of sin.
7 We know sin doesn't have power over dead people.
8 As surely as we died with Christ, we believe we will also live with him. 9 We know that death no longer has any power over Christ. He died and was raised to life, never again to die. 10 When Christ died, he died for sin once and for all. But now he is alive, and he lives only for God.
11 In the same way, you must think of yourselves as dead to the power of sin. But Christ Jesus has given life to you, and you live for God.
12 Don't let sin rule your body. After all, your body is bound to die, so don't obey its desires 13 or let any part of it become a slave of evil. Give yourselves to God, as people who have been raised from death to life. Make every part of your body a slave that pleases God.
14 Don't let sin keep ruling your lives. You are ruled by God's undeserved grace and not by the Law.Slaves Who Do What //Pleases God
15 What does all this mean? Does it mean we are free to sin, because we are ruled by God's gift of undeserved grace and not by the Law? Certainly not! 16 Don't you know that you are slaves of anyone you obey? You can be slaves of sin and die, or you can be obedient slaves of God and be acceptable to him. 17 You used to be slaves of sin. But I thank God that with all your heart you followed the example set forth in the teaching you received.
18 Now you are set free from sin and are slaves who please God.
19 I am using these everyday examples, because in some ways you are still weak. You used to let the different parts of your body be slaves of your evil thoughts. But now you must make every part of your body serve God, so that you will belong completely to him.
20 When you were slaves of sin, you didn't have to please God. 21 But what good did you receive from the things you did? All you have to show for them is your shame, and they lead to death. 22 Now you have been set free from sin, and you are God's slaves. This will make you holy and will lead you to eternal life. 23 Sin pays off with death. But God's gift is eternal life given by Jesus Christ our Lord.