TIT. 1
Salamu
1 Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa; 2 katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; 3 takalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu;
4 tkwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.Tito akiwa Krete
5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; 6 tikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. 7 tMaana imempasa askofut awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu; 8 bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;
9 takilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
10 Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. 11 tHao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu. 12 Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu. 13 tUshuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani; 14 twasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli. 15 tVitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia. 16 tWanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
TITUS 1
1 From Paul, a servant of God and an apostle of Jesus Christ.
I encourage God's own people to have more faith and to understand the truth about religion. 2 Then they will have the hope of eternal life God promised long ago. And God never tells a lie!
3 So, at the proper time, God our Savior gave this message and told me to announce what he had said.
4 t Titus, because of our faith, you are like a son to me. I pray that God our Father and Christ Jesus our Savior will be kind to you and will bless you with peace!What Titus Was To Do //in Crete
5 I left you in Crete to do what had been left undone and to appoint leaderst for the churches in each town. As I told you,
6 t they must have a good reputation and be faithful in marriage.t Their children must be followers of the Lord and not have a reputation for being wild and disobedient.
7 Church officialst are in charge of God's work, and so they must also have a good reputation. They must not be bossy, quick-tempered, heavy drinkers, bullies, or dishonest in business. 8 Instead, they must be friendly to strangers and enjoy doing good things. They must also be sensible, fair, pure, and self-controlled.
9 They must stick to the true message they were taught, so their good teaching can help others and correct everyone who opposes it.
10 There are many who don't respect authority, and they fool others by talking nonsense. This is especially true of some Jewish followers. 11 But you must make them be quiet. They are after money, and they upset whole families by teaching what they should not.
12 It is like one of their own prophets once said,
“The people of Crete
always tell lies.
They are greedy and lazy
like wild animals.”
13 This surely is a true saying. And you should be hard on such people, so you can help them grow stronger in their faith.
14 Don't pay any attention to any of those senseless Jewish stories and human commands. These are made up by people who won't obey the truth.
15 Everything is pure for someone whose heart is pure. But nothing is pure for an unbeliever with a dirty mind. That person's mind and conscience are destroyed. 16 Such people claim to know God, but their actions prove they really don't. They are disgusting. They won't obey God, and they are too worthless to do anything good.