Tito 2
Mafundisho ya kweli
1 Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho sahihi. 2 Waambie wanaume wazee kwamba wanapaswa kuwa na kiasi, wawe na busara na wataratibu; wanapaswa kuwa timamu katika imani yao, upendo na uvumilivu.
3 Hali kadhalika waambie wanawake wazee wawe na mwenendo wa uchaji wa Mungu; wasiwe wachongezi au watumwa wa pombe. Wanapaswa kufundisha mambo mema, 4 ili wawazoezeshe kina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto, 5 wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mambo ya nyumbani, na wawatii waume zao, ili ujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa.
6 Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi. 7 Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako. 8 Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili maadui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
9 Watumwa wanapaswa kuwatii wakuu wao na kuwapendeza katika mambo yote. Wasibishane nao, 10 au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonesha kwamba wao ni wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.
11 Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu wote. 12 Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia; tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu huu wa sasa, 13 tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo. 14 t Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
15 Basi, sema mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Titus 2
1 But speak thou the things which befit the sound doctrine:2 that aged men be temperate, grave, sober-minded, sound in faith, in love, in patience:3 that aged women likewise be reverent in demeanor, not slanderers nor enslaved to much wine, teachers of that which is good;4 that they may train the young women to love their husbands, to love their children,5 to be sober-minded, chaste, workers at home, kind, being in subjection to their own husbands, that the word of God be not blasphemed:6 the younger men likewise exhort to be sober-minded:7 in all things showing thyself an ensample of good works; in thy doctrine showing uncorruptness, gravity,8 sound speech, that cannot be condemned; that he that is of the contrary part may be ashamed, having no evil thing to say of us.9 Exhort servants to be in subjection to their own masters, and to be well-pleasing to them in all things; not gainsaying;10 not purloining, but showing all good fidelity; that they may adorn the doctrine of God our Saviour in all things.11 For the grace of God hath appeared, bringing salvation to all men,12 instructing us, to the intent that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly and righteously and godly in this present world;13 looking for the blessed hope and appearing of the glory of the great God and our Saviour Jesus Christ;14 who gave himself for us, that he might redeem us from all iniquity, and purify unto himself a people for his own possession, zealous of good works.15 These things speak and exhort and reprove with all authority. Let no man despise thee.